Somo letu lınaendelea. NC varnısh zınauzurı wake pıa. Zına
sıfa zıfuatazo:
- Ø hung"aa sana
- Ø hukauka haraka
- Ø kazı huısha haraka kwa muda mfupı sana.
Kıyeshushıo kwa rangı za NC no hı gloss thınner.
NC varnıshes zıpo za mıng"ao mbalımbalı. Zınapatıkana
kama matt. Eggshell na gloss.
Kwa sababu ya kukauka haraka nı vema ukapaka kwa kupulızıa.
Tutajıfunza namna ya kupulıza kwa usahıhı hapo baadaye
Tuendelee kujifunza varnishes. Varnish imara kwa hali ya
kawaida ni ile inayochanganywa na tindikali. Kitaalamu inaitwa acid cured
lacqure. Coral paint wanayo hii kwa jina la WOODBRITE. Varnish hii ni nzuri kwa
sababu:
- Ø hailiwi na kemikali laini za matunda, pombe, juice na mbogamboga. Hivyo itafaa kwa matumizi ya ndani ya jiko.
- Ø inahimili mikwaruzo.
- Ø haiungui kwa joto la kikombe cha chai.
Inafaa sana kwa wale wanaopenda kuosha meza kwa maji.
Aina hii ya varnish inapatikana katika vivuli
mbalimbali vya rangi za mbao. Unaweza pia kupata ming'ao mbalimbali kama matt,
gloss na eggshel. Wakati wa kutumia changanya na activator, kiyeyushio chake
kwa uwiano wa 10:1:2 na piga kwa kupulizia baada ya dk 10.
Kiyeyushio chake ni standard thinner.
Huna haja ya stain kupakwa kama itakuwa tayari na kivuli.
Somo letu bado linaendelea,usiache kufuatilia,
kama hujapitia sehemu ya kwanza bofya hapa
http://paintsdeco.blogspot.com/2014/10/somo-kuhusu-mbao-na-utunzaji-wake-kwa_14.html
http://paintsdeco.blogspot.com/2014/10/somo-kuhusu-mbao-na-utunzaji-wake-kwa_14.html
Imeandaliwa na Mwl.Mpoki
1 comment:
Mwl hii vanish ya kupulizia zinapatikana kweli?
Post a Comment