Pages

Tuesday, October 14, 2014

SOMO KUHUSU MBAO NA UTUNZAJI WAKE KWA KUTUMIA RANGI AU VANISHI-SEHEMU YA PILI

Somo letu lınaendelea. NC varnısh zınauzurı wake pıa. Zına sıfa zıfuatazo:
  • Ø  hung"aa sana
  • Ø  hukauka haraka
  • Ø  kazı huısha haraka kwa muda mfupı sana.


Kıyeshushıo kwa rangı za NC no hı gloss thınner.
NC varnıshes zıpo za mıng"ao mbalımbalı. Zınapatıkana kama matt. Eggshell na gloss.
Kwa sababu ya kukauka haraka nı vema ukapaka kwa kupulızıa. Tutajıfunza namna ya kupulıza kwa usahıhı hapo baadaye
Tuendelee kujifunza varnishes. Varnish imara kwa hali ya kawaida ni ile inayochanganywa na tindikali. Kitaalamu inaitwa acid cured lacqure. Coral paint wanayo hii kwa jina la WOODBRITE. Varnish hii ni nzuri kwa sababu:
  • Ø  hailiwi na kemikali laini za matunda, pombe, juice na mbogamboga. Hivyo itafaa kwa matumizi ya ndani ya jiko.
  • Ø  inahimili mikwaruzo.
  • Ø  haiungui kwa joto la kikombe cha chai.


Inafaa sana kwa wale wanaopenda kuosha meza kwa maji.

Aina hii ya varnish inapatikana katika vivuli mbalimbali vya rangi za mbao. Unaweza pia kupata ming'ao mbalimbali kama matt, gloss na eggshel. Wakati wa kutumia changanya na activator, kiyeyushio chake kwa uwiano wa 10:1:2 na piga kwa kupulizia baada ya dk 10.
Kiyeyushio chake ni standard thinner.

Huna haja ya stain kupakwa kama itakuwa tayari na kivuli.

Somo letu bado linaendelea,usiache kufuatilia,

Imeandaliwa na Mwl.Mpoki

1 comment:

ULAVO said...

Mwl hii vanish ya kupulizia zinapatikana kweli?