Pages

Tuesday, May 26, 2015

MAFUNZO YA FUNDI RANGIMIKOANI

Kampuni yetu imekuwa ikiendesha mafunzo mbalimbali hasa kwa mafundi Rangi,Kumekuwa hakuna sehemu maalum ya mafundi rangi kujifunza juu ya teknologia mpya ya upaka wa rangi.

Pia kumekuwa na bidhaa nyingi za rangi sokoni,Sasa ni Jukumu la fundi kumshauri sahihi mteja wake ili na yeye iwe rahisi kwake kufanya kazi hiyo na kazi yake iwe ni kazi ya kisasa na ya kupendeza.

Kama ninavyosema kila wakati kuwa upakaji wa rangi ni mfumo.Kwa hiyo mtumiaji(Fundi)lazima ajue ni mfumo gani ataweza kuutumia ili kufanya kazi yake(upakaji rangi)
Kwa kuyaona haya Ndio maana tunatoa mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kuitumia mifumo hiyo.

Hivi karibuni Mwl.Mpoki alikuwa anazunguka mikoani na nchi jirani kuwapatia ujuzi huu mafundi rangi.
Kama wewe ni Fundi na unahitaji kujifunza zaidi juu ya teknolojia mpya ya mifumo ya upakaji rangi,au una kampuni ya ujenzi na unahitaji mafundi wako wapate ujuzi huu basi usisite wasiliana nasi kwa mawasilianao yafuatayo
Mob:   0768 807 298
           0719 083 700
au barua pepe:paintsdecoration@gmail.com
pia unaweza kutembelea ukurasa wetu wa facebook:paintsdeco

Hizi ni baadhi ya picha katika semina hizo


Mafundi Rangi wakimsikiliza Mwl.Mpoki kwa makini

Sehemu ya semina ya mafundi Rangi

Wakati mwingine mazingira yanakuwa sio Rafiki sana kwa kujifunza lakini tunahakikisha kila aliyehudhuria kuna kitu anapata


Mwl.Mpoki akionyesha jinsi ya kuchanganya rangi

Fundi akijifunza jinsi ya kupaka rangi za Mchanga



Mtaalamu wa ufundi rangi Ndg.Frank Anthony akimuelekeza fundi jinsi sahihi ya kuchanganya Rangi
Hizi ni kazi walizozifanya mafundi katika mafunzo hayo


Picha ya Pamoja ya mafundi rangi waliohudhuria semina hiyo