Tunapaka rangi kwa lengo kubwa
moja, kulinda vifaa vya ujenzi vilivyo tumika kujenga majengo. Vifaa hivi
vimegawanyika makundi matatatu. mbao, metali na zege.
vifaa hivi huathiriiwa na mambo
ya mazingira kama joto, baridi, kemikali, vimelea na maji maji
Ziko njia nyingi za kuhifadhi
vifaa hivi, njia bora na rahisi ni kuvipaka rangi.
hebu tujiulize kwanza, tunalinda
dhidi ya nini? mazingira yana mambo mengi ambayo huathiri maisha ya binadamu na
vitu vilivyomo. kuwenye mazingira kuna joto, baridi, maji, kemikali na hewa
mbalimbali. ukivichunguza vitu hivi kwa makini utajua athari zake kwa vifaa vya
ujenzi.
Mbao huliwa na vimelea, huoza na
hupasuka jua linapokuwa kali. Chuma hutafunwa na kemikali kama vile tindikali,
alkali na chumvi. Kuta huliwa na vimelea na chumvi na kusababisha kupungua kwa
thamani yake.
Zipo namna nyingi za kufanya ili
kudhibiti hali hizo kutokea.
Wengine hutumia njia kadhaa kama hizi:
·
Mabati yaliyopakwa
rangi kabla
·
Vigae na marumaru
·
Vioo
·
Karatasi
·
Mawe.
Pamoja na kuwepo kwa vitu hivi
mbadala rangi ni kitu pekee na
rahisi kukitumia ili kuvihifadhi vifaa hivi.
Endelea kufuatilia mwendelezo wa somo hili wiki ijayo
Na Mwl.Mpoki.