Pages

Friday, November 22, 2013

SOMO KUHUSU RANGI-SEHEMU YA 3

Bado tunaendelea na mfululizo wa masomo yetu kuhusu rangi,Leo tuko sehemu ya tatu katika somo letu kuhusu rangi

Fuatana na Mwalimu uweze kujua kwa undani kuhusu rangi na baadae jinsi sahihi ya upakaji wa rangi

Kwangua vizuri nyuso zilizo athiriwa kisha paka dawa ya kuwaua kabisa kabla ya kuendelea kupaka rangi. Dawa hizi zipo aina mbalimbali km antifungal wash au biocidal wash.
Uso wenyewe pia ni uchafu. Hauna masikilizano na rangi hata kama ni msafi kwa kuuangalia. Ni vigumu kuuondoa na kuuosha  kwani ndio tunao upaka rangi. Utaratibu sahihi wa upakaji ndio suluhisho la uchafu huu.
Kuta zilizoharibiwa 

KWA NINI TUPAKE RANGI
Kuna  lengo kuu moja tu la kupaka rangi, ulinzi. Hata hivyo tunapolinda hujikuta tuna pamba pia.

ULINZI DHIDI YA NINI?
Kwenye mazingira kuna vitu kadhaa vinavyo weza kuathiri vifaa vyetu vya ujenzi. Vitu hivi hubadilili tabia za vifaa hivi na kuvipunguzia thamani. Vitu hivi ni kama vifuatavyo:
1.       Joto
2.       Baridi
3.       Maji
4.       Kemikali
5.       Ukungu
6.       Vimelea
7.       Hewa.

Kama hivi vinaweza kuathiri viumbe hai basi vitaharibu kabisa vifaa vya ujenzi iwapo havita dhibitiwa.
Matabaka ya rangi yaliyo pakwa kwa ustadi yanatosha kuweka uzio ili maadui hawa wasipenye.

Rangi haipakwi tu kwa mazoea kwa lengo la kulisafisha eneo kama wengine wanavyodhani, bali ni taaluma yenye kanuni maalumu. Kanuni hizi zikifuatwa vema, huleta matokeo yaliyokusudiwa. Kabla ya yote kanuni kuu ni kuusafisha uso usiwe na uchafu wowote kama ilivyo elekezwa hapo juu. Kanuni ya pili ni dhana ya uso ni uchafu na kutufanya tupake rangi kwa utaratibu ili ishike kwenye uso husika.

Kwa leo tunaishia hapa,usikose juma lijalo ambapo tunataelezea jinsi sahihi ya upakaji wa rangi