Wafuatiliaji wa Blog yetu leo,Mwalimu anaenda kutufundisha kitu cha muhimu sana katika rangi nacho ni utaratibu sahihi wa upakaji rangi,
Somo hili haliwahusu mafundi rangi peke yao bali ni mtu yeyote anaweza kujifunza somo hili,fuatana na Mwalimu katika mtiririko huu wa somo hili.Natumaini mpaka mwisho wa somo hili utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua taratibu sahihi za upakaji wa rangi
Tuanze sasa.......
1. Paka rangi sahihi ya kuanzia (primer)-
primer itafanya kazi zifuatazo:
·
Italeta
masikilizano kati ya uso na matabaka yanayo fuata.
·
Itaziba
nyufa na matundu madogomadogo yaliyopo kwenye uso.
·
Italeta
taswira ya uso ulivyo.
2. Ziba mabonde yaliyojitokeza kwa uwazi kwa
kijazio (putty) chenye gundi. Watengenezaji wamependekeza ya nje peke yake na ya
ndani peke yake. Zipo putty za mbao na chuma pia.
3. Paka rangi ya kuanzia tena.
4. Paka rangi ya kumalizia.
4. Paka rangi ya kumalizia.
Rangi ya kuanzia
hutegemea zaidi aina ya uso unaopakwa.
Lakini cha kuzingatia hapa ni wapi inapakwa, yaani mazingira husika. Kama
maeneo ni korofi au la. Kama eneo linachumvi, maji au kemikali isiyo koma,
umakini zaidi unahitajika katika uchaguzi wa rangi ya kuanzia. Watengenezaji
wanamapendekezo mbali mbali ya rangi za kuanzia kama inavyo ainishwa kwenye
jedwali lifuatalo.
Aina ya uso
|
Aina ya primer
|
kiyeyushio
|
mbao
|
Wood primer
|
Turpentine/solvent
|
Metali chuma
|
Red oxide primer
|
Turpentine/solvent
|
Zinc phosphate/zinc chromate
|
Turpentine/solvent
|
|
2k epoxy hb primer, zinc rich
|
Epoxy thinner
|
|
Metali si chuma
|
2k etch primer
|
hakuna
|
Primer zote za metali chuma
|
||
Kuta za zege, tofali, mawe, saruji
|
Acrylic primers
|
maji
|
Undercoats za mafuta
|
Turpentine/solvent
|
|
Pliolite based primers
|
Turpentine/solvents
|
.jpg)

1 comment:
Very good for this class byeee
Post a Comment