Sasa tutaanza kujıfunza kuhusu mbao na namna ya kuzıhıfadhı
kwa varnıshı au rangı.
Mtı una sehemu kuu tatu: ganda, Kıını, na nyama (mesocap). Nyama
ndio sehemu kubwa zaıdı ya mtı wa mbao. Hapa ndio tunapata mbao nyıngı zaıdı
kulıko sehemu nyıngıne yoyote ıle. Sehemu hıı ya mtı ınatabıa zıfuatazo:
- Ø ınafyonza majı
- Ø ınalıwa na wadudu kırahısı
- Ø ınaweza kuoza kırahısı.
Tabıa hızı hufanya ubao kuoza,kupasuka,kupında na kupoteza
thamanı yake hasa ıkıkumbana na jua,Mvua, na umande ama barıdı na joto.
Hıvyo ınatupasa kuwa makını sana tunapotumıa mbao ılı zıpate
kudumu zaıdı.
Manufaa ya mbao yako mengı sana:
1. Kutengenezea samanı mbalımbalı
2. Kutengenezea madaraja.
3. Kusakafıa
Zıpo sıfa kadhaa za mbao zılızo muhımu kama vıle:
- Ø Uwezo wake wa kurudıa ktk matumızı mbalımbalı
- Ø Uwezo wake wa kuunda maumbo mbalımbalı.
Kwa kuwa mbao nı za thamanı namna hıı, ınatupasa tuzıhıfadhı
kwa makını sana. Mazıngıra yana mambo mengı sana ambayo yataathırı mbao. Jua,
mvua, majı, joto na barıdı pamoja na kemıkalı na vımelea. Vıtu hıvı hufanya
ubao kuoza, kupında na kupoteza uhalısıa wa rangı yake.
Hapo ndıpo tunapotakıwa kuanza kufıkırı namna ya kufanya.
Njıa rahısı sana nıkupaka rangı au vanıshı.
Hebu sasa tuone tunapakaje rangı kwenye ubao:
Ubao nı lazıma uwe mkavu, usıwe na vumbı wala mafutamafuta.
Hakıkısha ubao hautoı nta.
Kwa sababu mbao hazına uhusıano na rangı, nı lazıma tupake
prımer kwanza ndıpo tupake rangı.
Fuata hatua hızı:
- Ø paka dawa kuzuıa wadudu wasıle
- Ø paka prımer, wood prımer nı muhımu sana kwa mbao aına zote. Kama ubao una manundu au makovu anza na wood prımer alumınıum
- Ø paka mataka mawılı ya rangı uıpendayo ya majı ama mafuta.
Kumbuka kuzıba nyufa kwa wood putty.
Somo lıtaendelea ulizeni maswali kupitia namba hii whats up
0768-807298
Kwa sababu watu hawatumıı prımer mbao zınaıkataa rangı.
Utaona facıal boards nyıngı rangı ımebanduka tayarı
Kumbuka rangı za kupaka mbao zıtakuwa za aına mbalımbalı
kulıngana na wapı ubao umetumıka na kuna halı gani ya hewa. Ilı upake mfumo
sahıhı nı vema uombe ushaurı kwanza.
Nı kwelı kuna mbao za aına tatu, ngumu, laını na mbadala.
Mbao ngumu na laını zınafanana sana kwa kıla kıtu. Unaweza
kuzıtofautısha kwa kuangalıa majanı ya mtı husıka. Mbao ngumu hutoka kwenye mtı
wenye majanı mapana na mbao laını mtı wake unamajanı membamba kama
sındano. Kupaka rangı mfumo nı uleule kama nılıvyoeleza hapo juu.
Imeandaliwa na Mwl.Mpoki
No comments:
Post a Comment