Pages

Monday, December 22, 2014

MAFUNZO YA UPAKAJI RANGI KWA VITENDO

Matayarisho kabla ya mafunzo kuanza

Fundi akichanganya rangi kabla ya kuanza kupaka ili kuhakikisha kuwa rangi imechanganyika vizuri 

Vifaa vinavyotumika ni pasi ya chuma na scraper





Mwalimu akisisitiza jambo katika utumiaji wa pasi


Mwl.Mpoki akielezea mafundi juu ya rangi hizo
















kwa mahitaji ya rangi hizi wasiliana nasi kwa namba 0719083700

Monday, November 24, 2014

BADILI MUONEKANO WA NYUMBA YAKO


Kuelekea Mwisho wa Mwaka watu wengi hupenda kubadili muonekano wa Nyumba zao,Kwa kuliona hilo Paintsdeco pamoja na kampuni mama ya Mpole coatings Limited tutaweletea namna mbalimbali za kubadili muonekano wa nyumba yako kupitia rangi.
Aina hizi za rangi ni ngeni nchini na kwa mafundi wengi,Ndio maana tumechukua jukumu la kufundisha mafundi jinsi sahihi ya kupaka rangi hizi.
usiwe na wasiwasi kama wewe ni fundi na unataka kujifunza jinsi sahihi ya kupaka rangi hizi wasiliana nasi .Na kama unataka kubadilisha muonekano wa Nyumba yako basi wasiliana nasi tunao mafundi wenye uzoefu wa kazi hizi.

The Art - Spatula




Ragged Stucco Metallic Gold

Ragged Stucco

Ragged Stucco Metallic

Ragged Stucco Metallic Bronze

Spatula



Ragging





Thursday, October 16, 2014

SOMO KUHUSU MBAO NA UTUNZAJI WAKE KWA KUTUMIA RANGI AU VANISHI-SEHEMU YA TATU

Aina nyingine ya varnish ni 2K PU varnish. Varnish hii ni imara sana kwa ajili ya ndani na nje. PU maana yake ni polyurathane.
Kazi kubwa ya kemikali hii ni kuzuia mionzi mibaya, kuimarisha isikwanguke na kuzuia joto na kemikali mbaya zisiharibu tabaka na ubao
Varnish hii ya 2k pu huchanganywa na hardener yake inaitwa 2k pu hardener na kiyeyushio chake 2k pu thinner kwa uwiano wa 4:1:2. Ni vema ukapulizia kila tabaka kila baada ya dakika kumi.
Unaweza kumaliza matabaka yote ndani ya masaa mawili. Baada ya hapo acha ikomae vema kwa muda wa siku tano mpaka saba ndipo uanze kutumia kifaa chako. Ukifanya hivyo faida zake zitakuwa kama ifuatavyo:

  • Ø  haita kwanguka 
  • Ø  haita liwa na kemikali
  • Ø  haita katikakatika
  • Ø  Mng"ao utadumu muda mrefu
  • Ø  haita ungua kwa joto la chai ama sefuria ikiwekwa juu yake.


Imeandaliwa na Mwl.Mpoki



Tuesday, October 14, 2014

SOMO KUHUSU MBAO NA UTUNZAJI WAKE KWA KUTUMIA RANGI AU VANISHI-SEHEMU YA PILI

Somo letu lınaendelea. NC varnısh zınauzurı wake pıa. Zına sıfa zıfuatazo:
  • Ø  hung"aa sana
  • Ø  hukauka haraka
  • Ø  kazı huısha haraka kwa muda mfupı sana.


Kıyeshushıo kwa rangı za NC no hı gloss thınner.
NC varnıshes zıpo za mıng"ao mbalımbalı. Zınapatıkana kama matt. Eggshell na gloss.
Kwa sababu ya kukauka haraka nı vema ukapaka kwa kupulızıa. Tutajıfunza namna ya kupulıza kwa usahıhı hapo baadaye
Tuendelee kujifunza varnishes. Varnish imara kwa hali ya kawaida ni ile inayochanganywa na tindikali. Kitaalamu inaitwa acid cured lacqure. Coral paint wanayo hii kwa jina la WOODBRITE. Varnish hii ni nzuri kwa sababu:
  • Ø  hailiwi na kemikali laini za matunda, pombe, juice na mbogamboga. Hivyo itafaa kwa matumizi ya ndani ya jiko.
  • Ø  inahimili mikwaruzo.
  • Ø  haiungui kwa joto la kikombe cha chai.


Inafaa sana kwa wale wanaopenda kuosha meza kwa maji.

Aina hii ya varnish inapatikana katika vivuli mbalimbali vya rangi za mbao. Unaweza pia kupata ming'ao mbalimbali kama matt, gloss na eggshel. Wakati wa kutumia changanya na activator, kiyeyushio chake kwa uwiano wa 10:1:2 na piga kwa kupulizia baada ya dk 10.
Kiyeyushio chake ni standard thinner.

Huna haja ya stain kupakwa kama itakuwa tayari na kivuli.

Somo letu bado linaendelea,usiache kufuatilia,

Imeandaliwa na Mwl.Mpoki

Friday, October 3, 2014

SOMO KUHUSU MBAO NA UTUNZAJI WAKE KWA KUTUMIA RANGI AU VANISHI


Sasa tutaanza kujıfunza kuhusu mbao na namna ya kuzıhıfadhı kwa varnıshı au rangı.

Mtı una sehemu kuu tatu: ganda, Kıını, na nyama (mesocap). Nyama ndio sehemu kubwa zaıdı ya mtı wa mbao. Hapa ndio tunapata mbao nyıngı zaıdı kulıko sehemu nyıngıne yoyote ıle. Sehemu hıı ya mtı ınatabıa zıfuatazo:
  • Ø  ınafyonza majı 
  • Ø  ınalıwa na wadudu kırahısı
  • Ø  ınaweza kuoza kırahısı. 


Tabıa hızı hufanya ubao kuoza,kupasuka,kupında na kupoteza thamanı yake hasa ıkıkumbana na jua,Mvua, na umande ama barıdı na joto.
Hıvyo ınatupasa kuwa makını sana tunapotumıa mbao ılı zıpate kudumu zaıdı.
Manufaa ya mbao yako mengı sana:
1. Kutengenezea samanı mbalımbalı
2. Kutengenezea madaraja.
3. Kusakafıa

Zıpo sıfa kadhaa za mbao zılızo muhımu kama vıle:
  • Ø  Uwezo wake wa kurudıa ktk matumızı mbalımbalı
  • Ø  Uwezo wake wa kuunda maumbo mbalımbalı.


Kwa kuwa mbao nı za thamanı namna hıı, ınatupasa tuzıhıfadhı kwa makını sana. Mazıngıra yana mambo mengı sana ambayo yataathırı mbao. Jua, mvua, majı, joto na barıdı pamoja na kemıkalı na vımelea. Vıtu hıvı hufanya ubao kuoza, kupında na kupoteza uhalısıa wa rangı yake.
Hapo ndıpo tunapotakıwa kuanza kufıkırı namna ya kufanya. Njıa rahısı sana nıkupaka rangı au vanıshı.

Hebu sasa tuone tunapakaje rangı kwenye ubao:
Ubao nı lazıma uwe mkavu, usıwe na vumbı wala mafutamafuta. Hakıkısha ubao hautoı nta.
Kwa sababu mbao hazına uhusıano na rangı, nı lazıma tupake prımer kwanza ndıpo tupake rangı.

Fuata hatua hızı:
  • Ø  paka dawa kuzuıa wadudu wasıle 
  • Ø  paka prımer, wood prımer nı muhımu sana kwa mbao aına zote. Kama ubao una manundu au makovu anza na wood prımer alumınıum 
  • Ø  paka mataka mawılı ya rangı uıpendayo ya majı ama mafuta.


Kumbuka kuzıba nyufa kwa wood putty.

Somo lıtaendelea ulizeni maswali kupitia namba hii whats up 0768-807298

Kwa sababu watu hawatumıı prımer mbao zınaıkataa rangı. Utaona facıal boards nyıngı rangı ımebanduka tayarı
Kumbuka rangı za kupaka mbao zıtakuwa za aına mbalımbalı kulıngana na wapı ubao umetumıka na kuna halı gani ya hewa. Ilı upake mfumo sahıhı nı vema uombe ushaurı kwanza.
Nı kwelı kuna mbao za aına tatu, ngumu, laını na mbadala.
Mbao ngumu na laını zınafanana sana kwa kıla kıtu. Unaweza kuzıtofautısha kwa kuangalıa majanı ya mtı husıka. Mbao ngumu hutoka kwenye mtı wenye majanı mapana na mbao laını mtı wake unamajanı membamba kama sındano.  Kupaka rangı mfumo nı uleule kama nılıvyoeleza hapo juu.

Imeandaliwa na Mwl.Mpoki



Monday, May 26, 2014

UTARATIBU SAHIHI WA UPAKAJI RANGI

Wafuatiliaji wa Blog yetu leo,Mwalimu anaenda kutufundisha kitu cha muhimu sana katika rangi nacho ni utaratibu sahihi wa upakaji rangi,
Somo hili haliwahusu mafundi rangi peke yao bali ni mtu yeyote anaweza kujifunza somo hili,fuatana na Mwalimu katika mtiririko huu wa somo hili.Natumaini mpaka mwisho wa somo hili utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua taratibu sahihi za upakaji wa rangi
Tuanze sasa.......

        1.       Paka rangi sahihi ya kuanzia (primer)- primer itafanya kazi zifuatazo:
·         Italeta masikilizano kati ya uso na matabaka yanayo fuata.
·         Itaziba nyufa na matundu madogomadogo yaliyopo kwenye uso.
·         Italeta taswira ya uso ulivyo.


2.     Ziba mabonde yaliyojitokeza kwa uwazi kwa kijazio (putty) chenye gundi. Watengenezaji wamependekeza ya nje peke yake na ya ndani peke yake. Zipo putty za mbao na chuma pia.

        3.       Paka rangi ya kuanzia tena.
        4.       Paka rangi ya kumalizia.

Rangi ya kuanzia hutegemea  zaidi aina ya uso unaopakwa. Lakini cha kuzingatia hapa ni wapi inapakwa, yaani mazingira husika. Kama maeneo ni korofi au la. Kama eneo linachumvi, maji au kemikali isiyo koma, umakini zaidi unahitajika katika uchaguzi wa rangi ya kuanzia. Watengenezaji wanamapendekezo mbali mbali ya rangi za kuanzia kama inavyo ainishwa kwenye jedwali lifuatalo.

Aina ya uso
Aina ya primer
kiyeyushio



mbao
Wood primer
Turpentine/solvent
Metali chuma
Red oxide primer
Turpentine/solvent

Zinc phosphate/zinc chromate
Turpentine/solvent

2k epoxy hb primer, zinc rich
Epoxy thinner
Metali si chuma
2k etch primer
hakuna

Primer zote za metali chuma

Kuta za zege, tofali, mawe, saruji
Acrylic primers
maji

Undercoats za mafuta
Turpentine/solvent

Pliolite based primers
Turpentine/solvents


Nafiki mpaka kufikia hapo msomaji wetu kuna kitu utakuwa umejifunza.
Mpaka wakati mwingine tuonane tena katika mwendelezo wa somo letu.

Friday, May 9, 2014

UCHAGUZI SAHIHI WA RANGI

Habari za siku nyingi wasomaji wa blog yetu,Tumekuwa kimya kutokana na majukumu .Mikutano ya mafundi Rangi sehemu mbalimbali ya nchi yetu.Kuanzia sasa tutakuwa tukiwafahamisha ni wapi mikutano ya mafundi rangi itakuwa ikifanyika katika mkoa wako.
hivi karibuni tuko mbioni kuandaa mkutano wa mafundi rangi wa mkoa wa Dar es salaam siku na mahali tutawajulisha.
Tutaomba fundi anayetaka kushiriki mafunzo hayo ya upakaji sahihi wa aina mbalimbali za rangi wajiandikishe mapema ili kupata idadi ya watakaoshiriki tukilinganisha na eneo.

Sasa turudi darasani kidogo!!!!

Ni upi uchaguzi sahihi wa rangi?
Swali hili nalielekeza kwa mwalimu
Fuatana naye ili ujue ni upi uchaguzi sahihi wa rangi.

Hii ni moja ya sehemu unayoyoweza kuchagua rangi


sehemu ya uchaguzi wa rangi chumbani

UPAKAJI WA RANGI ZA MAGARI

Fundi akipaka Putty