Pages

Friday, November 22, 2013

SOMO KUHUSU RANGI-SEHEMU YA 3

Bado tunaendelea na mfululizo wa masomo yetu kuhusu rangi,Leo tuko sehemu ya tatu katika somo letu kuhusu rangi

Fuatana na Mwalimu uweze kujua kwa undani kuhusu rangi na baadae jinsi sahihi ya upakaji wa rangi

Kwangua vizuri nyuso zilizo athiriwa kisha paka dawa ya kuwaua kabisa kabla ya kuendelea kupaka rangi. Dawa hizi zipo aina mbalimbali km antifungal wash au biocidal wash.
Uso wenyewe pia ni uchafu. Hauna masikilizano na rangi hata kama ni msafi kwa kuuangalia. Ni vigumu kuuondoa na kuuosha  kwani ndio tunao upaka rangi. Utaratibu sahihi wa upakaji ndio suluhisho la uchafu huu.
Kuta zilizoharibiwa 

KWA NINI TUPAKE RANGI
Kuna  lengo kuu moja tu la kupaka rangi, ulinzi. Hata hivyo tunapolinda hujikuta tuna pamba pia.

ULINZI DHIDI YA NINI?
Kwenye mazingira kuna vitu kadhaa vinavyo weza kuathiri vifaa vyetu vya ujenzi. Vitu hivi hubadilili tabia za vifaa hivi na kuvipunguzia thamani. Vitu hivi ni kama vifuatavyo:
1.       Joto
2.       Baridi
3.       Maji
4.       Kemikali
5.       Ukungu
6.       Vimelea
7.       Hewa.

Kama hivi vinaweza kuathiri viumbe hai basi vitaharibu kabisa vifaa vya ujenzi iwapo havita dhibitiwa.
Matabaka ya rangi yaliyo pakwa kwa ustadi yanatosha kuweka uzio ili maadui hawa wasipenye.

Rangi haipakwi tu kwa mazoea kwa lengo la kulisafisha eneo kama wengine wanavyodhani, bali ni taaluma yenye kanuni maalumu. Kanuni hizi zikifuatwa vema, huleta matokeo yaliyokusudiwa. Kabla ya yote kanuni kuu ni kuusafisha uso usiwe na uchafu wowote kama ilivyo elekezwa hapo juu. Kanuni ya pili ni dhana ya uso ni uchafu na kutufanya tupake rangi kwa utaratibu ili ishike kwenye uso husika.

Kwa leo tunaishia hapa,usikose juma lijalo ambapo tunataelezea jinsi sahihi ya upakaji wa rangi

Friday, November 8, 2013

SOMO KUHUSU RANGI-SEHEMU YA 2

KIPI KIFANYIKE ILI ULINZI UNAOTOKANA NA RANGI UWE WA UHAKIKA?Wengi wamekata tamaa baada ya kuona wamepaka rangi na muda mfupi tu inabanduka, inapasuka, inavimba na kuhariba kabisa. Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha haya, kubwa kuliko zote ni uchafu.Uchafu ni kitu chochote kile ambacho kitasababisha rangi isishike. Vitu hivi ni kama vumbi, unyevu, mafuta, kemikali,vimelea na uso wenyewe.

VUMBI         Lipo vumbi la aina mbili, la asili na la kujitakia. Vumbi la kujitakia ni kama vile unga wa gypsum, chokaa, nilu, saruji nyeupe, n.kVumbi huongeza nguvu ya utando (surface tension) kati ya uso unaopakwa rangi na rangi na kusababisha isishike au kuvimba.Utamaduni huu umeanza kuzoeleka miongoni mwa mafundi na matajiri wameona ni njia sahihi ya kupunguza gharama. Matokeo yake ni gharama kuongezeka, kurudia rudia kazi na kutopata matokeo sahihi yaliyokusudiwa.Ni lazima kuliondoa kwanza vumbi la aina yoyote ile kwenye uso kabla ya kuweka tabaka lolote lile.

MAJI MAJI AU UNYEVUNYEVUUchafu mwingine mbaya sana ni unyevu ndani au juu ya uso. Kwa sababu ni lazima upotee hewani huweza kuvimbisha na kuharibu tabia za tabaka. Rangi husukumwa na kuvimba, huondoa mng’ao na kuchelewesha ukaukaji. Ni lazima tuusubiri uso kukauka kabla ya kupaka rangi.Tutajuaje uso umekauka?Kwa sababu maji hutoka yaliko mengi kwenda yaliko kidogo (osmosis), njia rahisi ni kuyanasa yanayotoka.kwa karatasi ya nailoni yenye ukubwa wa mita moja kwa mita moja na kuibandika kwenye ukuta kwa gundi ya karatasi na kiacha kwa usiku mmoja. Kiasi cha maji yaliyo`yaliyonaswa yataamua ukuta umekauka au la.

CHUMVI CHUMVIChumvi hutafuna kuta, mbao, chuma na huathiri matabaka ya rangi. Huweza kubadilisha tabia za kivuli na kuiondoa rangi kabisa. Chumvi itokanayo na kukomaa kwa saruji ni rahisi kuidhibiti kuliko ile itokanayo na mchanga wa tofali au inayopandishwa na maji kutoka ardhini. Saruji hukomaa kwa muda wa siku ishirini na moja. Inapokomaa hutoa maji na chumvi ambayo hutwana kwenye uso wa lipu. Huu ni uchafu na ni lazima uondolewe.Sugua vizuri au kwangua hiyo chumvi kwa kikwangulio au pasi ya chuma. Paka primer sahihi tayari kwa kuweka matabaka.

VIMELEAFangasi, algae, bacteria, na vimelea vinginevyo vilivyomo kwenye nyuso mbalimbali navyo ni uchafu. Vinauwezo wa huharibu kuta na vifaa vingine kwa kuvipa muonekano mbaya. Bacteria huozesha kabisa. Vimelea hivi huota kwenye vifaa vya ujenzi kwa sababu vifaa hivi ni chakula. Maji na hewa vikiwepo vimelea huota na kushamiri na kasha hufa na kuacha sura mbaya juu ya nyuso

Endelea Kufuatilia mfulilizo wa somo hili:Na Mwl.Mpoki

Friday, October 11, 2013

MASOMO JUU YA RANGI YANAENDELEA

Kabla ya Chochote ni maelekezo,Mwalimu Mpoki akitoa maelekezo kabla ya kuingia kwenye vitendo


Sasa ni vitendo,Mafundi rangi za magari wakifanya kwa vitendo jinsi ya kupaka rangi za magari

Mwalimu akionyesha jinsi ya Kuchanganya Rangi

Hata wamama hawakubakia nyumba kwenye Kupata Ujuzi mpya juu ya Rangi











Sunday, October 6, 2013

SOMO KUHUSU RANGI

Tunapaka rangi kwa lengo kubwa moja, kulinda vifaa vya ujenzi vilivyo tumika kujenga majengo. Vifaa hivi vimegawanyika makundi matatatu. mbao, metali na zege.


vifaa hivi huathiriiwa na mambo ya mazingira kama joto, baridi, kemikali, vimelea na maji maji
Ziko njia nyingi za kuhifadhi vifaa hivi, njia bora na rahisi ni kuvipaka rangi.

hebu tujiulize kwanza, tunalinda dhidi ya nini? mazingira yana mambo mengi ambayo huathiri maisha ya binadamu na vitu vilivyomo. kuwenye mazingira kuna joto, baridi, maji, kemikali na hewa mbalimbali. ukivichunguza vitu hivi kwa makini utajua athari zake kwa vifaa vya ujenzi.



Mbao huliwa na vimelea, huoza na hupasuka jua linapokuwa kali. Chuma hutafunwa na kemikali kama vile tindikali, alkali na chumvi. Kuta huliwa na vimelea na chumvi na kusababisha kupungua kwa thamani yake.

Zipo namna nyingi za kufanya ili kudhibiti hali hizo kutokea. 
Wengine hutumia njia kadhaa kama hizi:
·         Mabati yaliyopakwa rangi kabla
·         Vigae na marumaru
·         Vioo
·         Karatasi
·         Mawe.


Pamoja na kuwepo kwa vitu hivi mbadala rangi ni kitu pekee na rahisi kukitumia ili kuvihifadhi vifaa hivi.

Endelea kufuatilia mwendelezo wa somo hili wiki ijayo
Na Mwl.Mpoki.

Friday, August 30, 2013

VIFAA VINAVYOTUMIKA KUPAKA RANGI ZA CORAL THE ART





NI VIZURI KUJIFUNZA

Katika kitu chochote kile ambacho unataka kukifanya kwa ufanisi zaidi lazima ujifunze juu ya kitu hicho,
Leo tumekutana na mafundi rangi ambao walikuwa wakijifunza juu ya upakaji wa rang mpya iliyoingia sokoni kwa sasa,
Rangi hiyo Mpya inaitwa Coral the Art inayoyengenezwa na kiwanda cha kutengeneza rangi nchini cha Insignia Ltd.

Pichani ni mafundi waliokuwa kwenye mafunzo hayo ya vitendo ya siku 3

Hii ndio bidhaa mpya ya Rang kutoka kwa kampuni ya Insignia Ltd



Fundi akipaka Base cort
Mwalimu akimuelekeza Fundi jinsi ya upakaji Sahihi
Mwalimu akiangalia kazi iliyofanywa na moja ya fundi
Mwalimu akitoa maelekzo kwa mafundi na wao wako makini kumsikiliza
Mafunzo yanaendelea
Fundi akimalizia kupaka Top Cort



ONA MATOKEO YA CORAL THE ART













Sunday, July 28, 2013

SI WATU WENGI WANAFAHAMU RANGI NI NINI. KAMA WEWE NI FUNDI HEBU JARIBU ILI SOMO LETU LIANZIE HAPO




Kitu chochote kile kikipakwa sehemu kikashika na kufunika kitaitwa rangi. na ili hili litokee rangi imetengenezwa na gundi, kiasili cha rangi, kimiminika na kiambatanishi.

Tunapaka rangi kwa lengo kubwa moja, kulinda vifaa vya ujenzi vilivyo tumika kujenga majengo. Vifaa hivi vimegawanyika makundi matatatu. mbao, metali na zege.

vifaa hivi huathiriwa na mambo ya mazingira kama joto, baridi, kemikali, vimelea na maji maji.


Ziko njia nyingi za kuhifadhi vifaa hivi, njia bora na rahisi ni kuvipaka rangi.

Thursday, July 11, 2013

UZURI WA TANZANIA

Mungu ametupendelea Tanzania kuwa na mazingira na mandhari nzuri za kupendeza karibu katika kila mkoa wa Tanzania Bara na Visiwani.
Uzuri huo ambao Mungu ametujaalia tunaweza kuwa nao karibu kabisa katika mazingira tunayoishi na sisi tukawa ni sehemu ya uzuri huo


Picha hii inaonyesha sehemu ya mlima Kilimanjaro ni sehemu ya uzuri wa tanzania.